Matumizi ya Alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatoa wito kwa
Taasisi za Serikali kuhakikisha kuwa zinatumia alama za Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC) ambazo ni Bendera na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Alama hizo zinatakiwa kutumika kwenye Ofisi za Serikali
(Wizara, Idara zinazojitegemea, mashirika ya umma na Wakala) sambamba na alama za Taifa yaani Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wimbo wa Taifa.
Bendera ya Jumuiya inatakiwa kupepea sambamba na Bendera ya Taifa kwenye Ofisi za Serikali na Wimbo wa Jumuiya nao unatakiwa kuimbwa sambamba na Wimbo wa Taifa wakati wa shughuli rasmi za Kiserikali.
Hatua
hiyo ni utekelezaji wa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambao katika kifungu cha
7(a) umesisitiza Jumuiya hii kuwa ni
Jumuiya ya watu, hivyo wananchi wa Tanzania watahusishwa katika hatua
zote za Mtangamano. Aidha, Serikali
ya awamu ya tano
(5) chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki itahakikisha
kuwa Watanzania wanashirikishwa kikamilifu katika hatua mbalimbali za
Jumuiya ili kuijua kwa madhumuni ya kunufaika na fursa mbalimbali
zinazopatikana ndani ya Jumuiya hiyo.
Matumizi ya alama
hizi ni njia mojawapo ya kujenga uzalendo na kumfanya Mwananchi
ajisikie kuwa sehemu ya Ushirikiano huu. Aidha, Taasisi binafsi hasa
Mashule na Vyuo wanasisitizwa kutumia alama hizi kama sehemu ya
kuelimisha na kuhamasisha vijana kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaratibu zoezi la
upatikanaji wa sampuli ya alama hizo kwa gharama za taasisi husika,
hivyo Wizara, Taasisi na Ofisi za Serikali zinahimizwa kuwasiliana na
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya
ufafanuzi zaidi wa upatikanaji na matumizi ya alama hizo.
Mkurugenzi wa Masomo katika Chuo cha Diplomasia, Dkt. Watengere Kitojo naye akizungumza kuhusu Kozi zinazotolewa na chuo hicho ikiwemo Cheti, StaShahada, Shahada katika masuala ya Uhusiano wa Kimataifa |
Au unaweza kutuma maelezo ya Press Card yako, picha ya ndogo (passport size) kwenye email ifuatayo; media@eachq.org, CC:oothieno@eachq.org.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 19 Mei 2016.