EAST AFRICA YOUTH TANZANIA

EAST AFRICA YOUTH TANZANIA

Friday, July 1, 2016

ITAMBUE JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA FURSA ZITOKANAZO NA UMOJA WA FORODHA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Taasisi ya Kiserikali

 

(inter-Governmental Organization), iliyoanzishwa

na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Mkataba

ulianzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ulisainiwa

tarehe 30 Novemba, 1999 na ulianza kutumika

rasmi mnamo tarehe 7 julai 2000. Nchi za Rwanda

na Burundi zilijiunga katika Jumuiya ya Afrika

Mashariki mwaka 2007.

Jumuiya ya awali ya Afrika ya Mashariki iliundwa

mwaka 1967 na kuvunjika mwaka 1977. Kuvunjika

kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977

kulitokana na sababu nyingi zikiwemo za kisiasa,

kijamii na kimaslahi. Sababu hizo ni pamoja na:

 

a. Itikadi tofauti za kisiasa zilizokuwa zikifuatwa

na Nchi Wanachama

 

b.Kutoelewana katika mgao wa mapato kutoka

katika Mashirika ya huduma za Pamoja na

kutokuwepo kwa Seraya kushughulikia tatizo

hilo;

c.Athari za vita baridi baina ya Amerika na

Urusi kwa wakati huo;

 

d.Ushiriki mdogo wa sekta binafsi na vyama

vya kiraia katika uendeshaji wa Jumuiya ;

na

e. Mtizamo finyu kuhusu mtangamano kwa

baadhi ya viongozi na watendaji.

Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya, Nchi Wanachama

zilitiliana saini makubaliano ya kugawa mali na

madeni (mediation agreement for the divisionof assets

 

amhuri

 

ya

m

uungano

•Tanzania • B

No comments:

Post a Comment