EAST AFRICA YOUTH TANZANIA

EAST AFRICA YOUTH TANZANIA

Friday, July 1, 2016

Alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Matumizi ya Alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatoa wito kwa Taasisi za Serikali kuhakikisha kuwa zinatumia alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo ni Bendera na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Alama hizo zinatakiwa kutumika kwenye Ofisi za Serikali (Wizara, Idara zinazojitegemea,  mashirika ya umma na Wakala) sambamba na alama za Taifa yaani Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wimbo wa Taifa. 
Bendera ya Jumuiya inatakiwa kupepea sambamba na Bendera ya Taifa kwenye Ofisi za Serikali na Wimbo wa Jumuiya  nao unatakiwa kuimbwa sambamba  na Wimbo wa Taifa wakati wa shughuli rasmi za Kiserikali. 
Hatua hiyo ni utekelezaji wa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao katika kifungu cha 
7(a) umesisitiza Jumuiya hii kuwa ni Jumuiya ya watu, hivyo wananchi wa Tanzania watahusishwa katika hatua zote za Mtangamano. Aidha,  Serikali ya awamu ya tano 
(5) chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki itahakikisha kuwa Watanzania wanashirikishwa kikamilifu katika hatua mbalimbali za Jumuiya ili kuijua kwa madhumuni ya kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya Jumuiya hiyo.
Matumizi ya alama hizi ni njia mojawapo ya kujenga uzalendo na kumfanya Mwananchi ajisikie kuwa sehemu ya Ushirikiano huu. Aidha, Taasisi binafsi hasa Mashule na Vyuo wanasisitizwa kutumia alama hizi kama sehemu ya kuelimisha na kuhamasisha vijana kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaratibu zoezi la upatikanaji wa sampuli ya alama hizo kwa gharama za taasisi husika, hivyo Wizara, Taasisi na Ofisi za Serikali zinahimizwa kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya ufafanuzi zaidi wa upatikanaji na matumizi ya alama hizo.

Mkurugenzi wa Masomo katika Chuo cha Diplomasia, Dkt. Watengere Kitojo naye akizungumza kuhusu Kozi zinazotolewa na chuo hicho ikiwemo Cheti, StaShahada, Shahada katika masuala ya Uhusiano wa Kimataifa
Au unaweza kutuma maelezo ya Press Card yako, picha ya ndogo (passport size) kwenye email ifuatayo; media@eachq.org, CC:oothieno@eachq.org.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 19 Mei 2016.

ITAMBUE JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA FURSA ZITOKANAZO NA UMOJA WA FORODHA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Taasisi ya Kiserikali

 

(inter-Governmental Organization), iliyoanzishwa

na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Mkataba

ulianzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ulisainiwa

tarehe 30 Novemba, 1999 na ulianza kutumika

rasmi mnamo tarehe 7 julai 2000. Nchi za Rwanda

na Burundi zilijiunga katika Jumuiya ya Afrika

Mashariki mwaka 2007.

Jumuiya ya awali ya Afrika ya Mashariki iliundwa

mwaka 1967 na kuvunjika mwaka 1977. Kuvunjika

kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977

kulitokana na sababu nyingi zikiwemo za kisiasa,

kijamii na kimaslahi. Sababu hizo ni pamoja na:

 

a. Itikadi tofauti za kisiasa zilizokuwa zikifuatwa

na Nchi Wanachama

 

b.Kutoelewana katika mgao wa mapato kutoka

katika Mashirika ya huduma za Pamoja na

kutokuwepo kwa Seraya kushughulikia tatizo

hilo;

c.Athari za vita baridi baina ya Amerika na

Urusi kwa wakati huo;

 

d.Ushiriki mdogo wa sekta binafsi na vyama

vya kiraia katika uendeshaji wa Jumuiya ;

na

e. Mtizamo finyu kuhusu mtangamano kwa

baadhi ya viongozi na watendaji.

Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya, Nchi Wanachama

zilitiliana saini makubaliano ya kugawa mali na

madeni (mediation agreement for the divisionof assets

 

amhuri

 

ya

m

uungano

•Tanzania • B

MH. RICHARD KASESELA IRINGA DC KATIKA MAHAFARI YA EAST AFRICA CHUO KIKUU RUCU

Mkuu wa Wilaya ya Iringa DC Mhe Richard Kasesela

Leo alikuwa mgeni Rasmi katika mahafari  ya EASTAFRICA COMMUNITY EAC katika chuo kikuu RUCU

Ambapo ametoa  ushauri kwa wanafunzi kwa habari ya uwekezaji kipindi wakiwa shule mfano kwa Iringa kuna fursa ya upandaji Miti.

Kipindi anajibu RISALA Mhe. Mkuu wa Wilaya Richard Kasesela anasema kuandaa mpango kazi kwa lengo la kufanikisha malengo ya jumuiya ya UMOJA wa Africa Mashariki katika chuo cha RUCU. Pia ( fundarising proposal) 

kwa upande wa vyuo vikuu pia ametoa ushauri kuandaa mashindano ya vyuo vya hapa iringa mjini kwa lengo la kufanya Iringa kuwa kituo cha maarifa." Center of Knowledge "

Pia kwa upande wa Mchungaji ameongelea Misingi ya Maadili ni katika uchaji wa UPENDO, UMOJA,MSHIKAMANO NA AMANI 



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Jumuiya ya Afrika Mashariki

Jumuiya ya Afrika Mashariki au Mtangamano wa Afrika Mashariki (kwa Kiingereza East African Community, kifupi EAC)



Ni muundo wa kisiasa unaounganisha nchi tano za kanda ya Maziwa Makuu ya Afrika Mashariki: Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. Mnamo Machi 2016 Sudan Kusini imekuwa nchi wa sita.
Eneo la Mtangamano ni 1,820,664 square kilometres (702,962 sq mi), likiwa na wakazi 153,301,178 (kadirio la mwaka 2014)
Jumuiya yenye jina hilo imepatikana mara mbili katika historia: jumuia ya nchi tatu kubwa zaidi kati ya hizo ilianzishwa mwaka 1967, lakini ilisambaratika mwaka 1977
Jumuiya ilifufuliwa rasmi tarehe 7 Julai 2000.