Kiasi cha $30 milioni zitaisaidia moja kwa moja Sekretarieti ya EAC
Secretariat, ilhali kitakachobaki kitagharamia wadau wengine wa kikanda katika
juhudi zao za kuendeleza ajenda ya EAC ya utangamano kikanda.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania na EAC Virginia Blaser, Mkurugenzi wa USAID wa Kenya na Afrika Masharika
Karen Freeman, na Katibu Mkuu wa EAC Balozi Liberát Mfumukeko walitia saini
hati ya makubaliano.
Kaimu Balozi Blaser alitambua manufaa makubwa ya kukuza ushirikiano wa
kikanda, akielezea kuwa Marekani inaunga mkono “serikali na mashirika ya kikanda
kama EAC katika juhudi zao za pamoja kufungua fursa zilizopo za kikanda kwa
manufaa ya watu wake,”
Mkurugenzi wa USAID Freeman alisisitiza
mafanikio ya pamoja ya EAC na USAID katika miongo miwili iliyopita. “Kwa
kurahisisha utaratibu wa forodha na mipaka, tumerahisisha kasi, gharama nafuu
na biashara ya uhakika. Tumeongeza uwekezaji kwa kufanikisha mikataba ya
kimataifa ambayo inakuza viwanda vya ndani na vya uzalishaji.”
Kwa
makubaliano haya, jumuiya ya EAC na Marekani zitafanya kazi kwa pamoja kwa (i) kuendeleza
utangamano wa kiuchumi kikanda, (ii) kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi
wanachama na Marekani, (iii) kuboresha usimamizi endelevu wa maliasili katika
Ziwa Victoria na mfumo wa ikolojia wa Mto Mara, (iv) kuboresha upatikanaji wa
huduma ya afya ya pamoja maeneo ya mipakani na (iv) kuimarisha mpangilio wa
uongozi wa EAC.
Kupata taarifa zaidi kuhusu taarifa hii, tafadhali
wasiliana na Ubalozi wa Marekani Ofisi ya Habari simu: +255-22-229-4000 au
baruapepe:
DPO@state.gov.